Sunday, July 20, 2014

TAPELI LILILOJIDAI KISHOKA WA TANESCO LADAKWA LIVE MLIMANI CITY

10500539_819006161445574_7780628803053090260_n
Pichani juu na chini ni Kishoka wa Tanesco aliyekamatwa Mlimani City.
Na Mwandishi wetu

TAPELI lililokubuhu kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya kishoka washirika la Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya kuwekewa mtego walipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma- Ledama.

Kwa mujibu wa Bi. Usia akieleza tukio hilo, alidai kuwa tapeli huyo alifika asubuhi akiwa na wenzake sita, nyumbani kwake wakasema wanatoka Tanesco wamekuja kucheki mita ya Luku. Hata hivyo wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na kung'oa mita, eti waliona kwenye GPS yao kuwaUmeme hauendi vema.

“wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia. nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwamwezi? si ingepaswa tulipe kidogo? wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa kinafyatuka halafu Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia.

Na kuongeza kuwa vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka, tujipange. tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu wanalazimisha mambo, wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki. tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuitePolisi, basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie Umeme, mengine Jumatatu. wakaja fasta wakarudisha Umeme, nikawaambia naenda aTM wasubiri nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka Polisi chuo nikawahadithia wakanipa Polisi 3 nikaja nao nyumbani, tukawakuta wameondoka.

Mzee akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City, tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. tumemuacha selo, tukaandikisha maelezo.

10417599_819006198112237_2101442257557265538_n  
Hapa likiwa chini ya ulinzi na pingu mkononi.

Usahihi wa taarifa ya kuungua kwa Jengo la Naura Springs Hotel Arusha.

naura-spring-hotelKama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii bila shaka utakuwa umekutana na picha ambayo inaonyesha hotel ya Naura ikiungua moto huku nyingi zikionyesha moto wake umeshika kasi kwenye kuwaka.

Baada ya kusambaa kwa picha hizo www.shakoorjongo.blogspot.com ilimtuma mwakilishi wake kutoka Arusha kwa ajili ya kwenda kupata uhakika wa taarifa hizi ambazo amesema kuwa si za kweli na hata uongozi na wafanyakazi wa hotel hiyo wameshangazwa na picha hiyo. 

Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi wa kujua haswa picha hiyo ilipoanzia kusambaa ili kuweza kuwatambua walioanza kuzisambaza picha hizo.

nauraaa

DIAMOND ASHIRIKI UZINDUZI WA FILAMU YA THINK LIKE A MAN


Msanii Diamond Platnumz akihojiwa wakati wa uzinduzi wa filamu ya THINK LIKE A MEN.


Msanii Diamond,pamoja na wageni alioambatana nao akiwemo Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba wakati wakiwasili katika uzinduzi huo.


Terrence akizungumza kabla ya uzinduzi wa filamu ambayo naye ameshiriki kuanza.


Diamond akisalimiana na baadhi ya mashabiki baada ya uzinduzi.

DOGO JANJA AMUOMBA MSAMHA MADEE

Mwanamuziki wa Bongofleva pichani hivi karibuni alimuomba msamaha Madee na kurudishwa rasmi katika kundi la Tip Top Connection

Sunday, July 13, 2014

TRACY MORGAN ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI

Tracy Morgan.
STAA wa vichekesho nchini Marekani, Tracy Morgan, ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kukaa wiki tano tangu alipopata ajali iliyomuua mwenzake Jimmy Mack.
Morgan alivunjika mguu na mbavu baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongwa kwa nyuma huko New Jersey, Marekani Juni 7 mwaka huu.
Katika ajali hiyo, mchekeshaji James McNair, maarufu kwa jina la Jimmy Mack alifariki dunia huku mchekeshaji Ardley Fuqua na abiria mwingine aitwaye Jeffrey Millea, wakijeruhiwa.