Meneja wa Mirror na wasanii wa Endless
Fame, Petit Man, amefunga ndoa ya Kiislamu na dada wa msanii wa Bongo
Fleva, Diamond Platnumz aitwaye Esma usiku wa kuamkia leo.
Sunday, September 21, 2014
MSANII BONGO FLEVA AAIBISHA MA-MISS
Msanii wa kitambo wa Bongo Fleva aliyewahi kutamba na Kundi la Chamber Squad na ngoma yake ya taifa ya Kama Vipi, Moses Bushagama ‘Mez B’ anadaiwa kuwaaibisha ma-miss kwa kuwalazimisha kupiga nao picha wakiwa watupu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, jamaa huyo aliwafuata warembo hao waliojitambulisha kwa majina ya Vicky na Rebecca waliokuwa kwenye swimming pool (bwawa la kuogelea) ambao ilisemekana kuwa siyo raia wa Bongo na huko wanakotokea ni ma-miss.
Ilidaiwa kwamba Mez B ndiye aliyewaomba kupiga nao picha lakini jamaa huyo ‘akaharibu’ baada ya kwenda mbele zaidi na kuanza kuwaminya ‘vifuu’ vyao kifuani vilivyoonekana ni vya saa sita vilivyokuwa wazi bila hata ‘braa’.
Ilisemekana kwamba baada ya kupiga picha hizo, yeye (Mez B) aliwafowadia washikaji zake ndipo zikazagaa kupitia mtandao wa WhatsApp.
“Hawa wasanii wetu kweli ni majanga. Ona Mez B alichokifanya na hawa mabinti. Yaani wapo kama walivyozaliwa lakini yeye yupo freshi na nguo zake. Kama siyo kudhalilishana ni nini! Amewaaibisha sana. Lakini na wao hawakuona?” alihoji mrembo mmoja aliyefowadiwa picha hizo na rafiki yake kwenye WhatsApp.
Baada ya kuzitia picha hizo kibindoni, gazeti hili lilimtafuta Mez B kisha kumbana kuhusu tukio hilo ambapo alijitetea kwa ufupi:“Wale ma-miss walikuwa wanaogelea vifua wazi kwa muda mrefu. Wao ndiyo walioniomba kupiga nao picha.”
Kumekuwa na kasumba ya kupiga picha za utupu kisha kuziachia mtandaoni kwa kudhani kuwa ni kujiongezea umaarufu lakini ukweli ni kujiondolea utu na heshima mbele ya jamii.
Monday, September 8, 2014
JIHAN DIMESH AWA REDD’S MISS ILALA 2014
MREMBO JIHAN DIMESH juzi
usiku aliibuka Redd’s Miss Ilala 2014 katika kinyang’anyiro
kilichofanyika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam
na kushirikisha wanyange kumi.
MADAWA YA KULEVYA: DIAMOND KIMENUKA
NIkweli kimenuka! Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yupo kikaangoni, habari zinadai kwamba kila anaponyanyua miguu, kikosi cha kupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini chini ya kamishna wake, Godfrey Nzowa nao wananyanyua miguu yao kumfuatilia, Amani limesheheni.
Akizungumza na wanahabari wetu jijini Dar, Jumatatu iliyopita, afisa mmoja wa ngazi ya juu wa kitengo hicho ambaye hakupenda kuchorwa jina gazetini, alisema Diamond amepewa maelekezo yote muhimu.
MAELEKEZO ALIYOPEWA
“Tumempa maelekezo Diamond, atuletee mikataba ya shoo zote anazokwenda kuzifanya nje ya nchi ili tujiridhishe kama kweli ni halali au anakwenda kwa ajili ya biashara nyingine.
“Hiyo yote inatokana na uchunguzi wetu kwake kuhusu akaunti zake za benki kuonesha kwamba ana fedha nyingi sana zinazotia shaka kama amezipata kihalali,” alisema afisa huyo.
KUNUNUA NYUMBA
Afisa huyo aliendelea kusema kwamba, uchunguzi wao pia umebaini kwamba, msanii huyo wa Bongo amekuwa akinunua nyumba kila anaporejea kutoka kwenye shoo zake nje ya nchi, jambo ambalo taasisi haiamini kama kweli analipwa pesa nyingi kwa shoo moja, kiasi cha kumwezesha kununua nyumba jijini Dar.
“Tumebaini kwamba Diamond kila akirudi nchini kutoka kwenye shoo zake hununua nyumba. Analipwa kiasi gani cha fedha kule kwenye shoo? Hapa ndipo tunaposimamia sisi,” alisema afisa huyo huku akigongea msumari kuwa Diamond mwenyewe amekatazwa kuzungumza kwenye vyombo vya habari kuhusu kutakiwa kuwasilisha mikataba ya shoo zake za nje.
KUNA UKWELI?
Amani lilifuatilia na kubaini kwamba, Diamond aliporejea kutoka kwenye safari yake ya Marekani hivi karibuni, alinunua nyumba kwa Sh. milioni 80 iliyopo maeneo ya Mwananyamala-Magengeni, Dar.
Siku za nyuma, msanii huyo aliwahi kuripotiwa kununua nyumba zaidi ya mbili maeneo ya Kijitonyama, Dar, kiasi cha kuandikwa na vyombo vya habari kwamba amenunua mtaa.
KUHUSU AKAUNTI YA BENKI
Diamond mwenyewe aliwahi kuhojiwa katika Kipindi cha Take-One kinachorushwa hewani na CloudsTV ambapo alipoulizwa akaunti yake inasomaje, alijibu kuwa ina zaidi ya bilioni moja hivi.
DONDOO ZA UWEZO WA DIAMOND
1. Ana utajiri unaozidi shilingi bilioni 1.
2. Yupo kwenye mazungumzo na promota wa Rwanda kufanya shoo moja ya uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 (zaidi ya Sh. milioni 190).
3. Malipo ambayo hupokea kwa shoo zake nyingi za nje ya nchi hayashuki chini ya dola 25,000 (zaidi ya Sh. milioni 40).
4. Tangu mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya Sh. milioni 100.
5. Anamiliki nyumba kadhaa jijini Dar ambazo amepangisha watu.
6. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake, Papa Misifa ilibidi amlipe Sh. milioni 18.
NZOWA AZUNGUMZA NA AMANI
Gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Nzowa ambapo alipopatikana na kuulizwa, alisema:
“Ni kweli! Sisi kila mtu mwenye kipato cha kutia shaka lazima tumchunguze. Diamond kama ana mali zote kwa nini tusimchunguze. Ikithibitika anajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ama zake ama zetu huo ndiyo utaratibu wetu.”
DIAMOND SASA
Amani lilimsaka Diamond na kumuuliza kama analijua kasheshe hilo ambapo alisema:
“Najua, ila nimegundua kuna watu wamepanga kunishusha chini kisanii ndiyo wanaoeneza taarifa kwamba mimi nasafirisha unga.”
Amani: Sasa unadhani kwa nini hao watu unaosema wamependa kukushusha kisanii wasitumie njia nyingine, hasa ya sanaa wakatumia hiyo ambayo unasema si kweli?
Diamond: We elewe hivyo kaka (akakata simu).
SAFARI ZA NJE
Kwa kipindi kirefu sasa Diamond ambaye ni mpenzi wa Wema Isaac Sepetu, amekuwa akisafiri nchi mbalimbali kwa shoo na mambo binafsi ambapo mbali na nchi kibao za Bara la Afrika, ameshasafiri nchi nyingi zikiwemo Marekani, Uingereza, China, Norway, Ujerumani, Dubai na nyinginezo.
Stori: Shakoor Jongo
AJALI YA GARI YAUA MBEZI JIJINI DAR
KESI YA PONDA YAAHIRISHWA MPAKA SEPTEMBA 22
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 22 Septemba mwaka huu. Aidha Shehe Ponda aliwaasa waumini wanaomuunga mkono watume wawakilishi wachache kesi hiyo itafanyika katika chumba maalum kijulikanacho kama ‘chamber court’.
YALIYOJIRI MAHAKAMA YA MWANZO KINONDONI LEO
Subscribe to:
Posts (Atom)